SEASON TWO 01 HADI 03
KIPENGELE CHA 01
Siku zilikuwa zimesogea, miezi 26 ikakatika, na miaka miwili ikawa imeshapita.
Tricia alikuwa ameshamaliza chuo mwaka wa tano, Muhimbili na alikuwa kwenye gari kuelekea mbeya kwani ndipo alipotakiwa kwenda kufanya internship (mafunzo ya matendo) kwa mwaka mmoja katika hospitali ya rufaa ya Mkoa wa Mbeya.
Mkononi binti alikuwa ameshikilia simu aina ya iPhone 13 Pro Max, na wala alikuwa haringi, mtoto kwao pesa ilikuwepo.
Alimtumia ujumbe mtu mmoja akamueleza “Nikifika nitakukumbatia kwa nguvu” yule mtu akamjibu
“Daah....nakusubiri kwa hamu kubwa...leo utalala kwangu ama utalala lodge?” aliuliza huyo kijana
“Nitalala lodge tena peke yangu” alisema Tricia
“Weee.....sio tupumzike wote?”
“Maswali gani hayo Frank? Mi nimeamua kufanya Mbeya ili tupate muda wa kuwa karibu...sasa unahisi nataka kulala wapi? Sio kulala tu siku moja, mara nyingi tu nitakuwa nalala kwako. Au hutaki?”
“Nataka sasa”
“Haya....niko njiani nakuja mpenzi”
“Sawa”
Ni dhahiri kwamba Tricia alikuwa ameshaingia kwenye mahusiano na mwanaume mwingine aitwaye Frank Bukuku, na alikuwa ameshamsahau kabisa Maulid. Mapenzi yake na mwaka yalikuwa ndo yameshanoga na walikuwa pamoja kwa kipindi cha miezi tisa. Binti hakuwa na mpango tena na Maulid licha ya kuangukia katika mapenzi kwa kipindi cha miaka miwili iliyokuwa imepita.
Maulid alikuwa mbali, alikuwa hana mawasiliano naye kabisa na siku zote mapenzi bila mawasiliano huwa yanaisha, hivyo Tricia aliona namba ya Maulid imeshafungiwa na mtandao, basi aliifutilia mbali na kuamua kuanza mapenzi mapya na mwanaume mwingine ambaye alikuwa akisoma naye chuo cha udaktari Muhimbili.
*
Ilipofika muda wa saa mbili jioni mzee Mwaipopo ambaye ni baba yake Tricia, alikuwa pamoja na mke wake Bi Grace ambaye pia ni mama Tricia, walikuwa na mtoto wao mdogo aitwaye Providence. Wakati huo dada yake Providence ambay ni Caroline alikuwa amepelekwa shule ya kulala iitwayo Tanganyika International School.
Wakati baba amempaka Providence, alikuwa akijadiliana na mama
“Kwa hiyo isingewezekana yeye kufanya internship katika hospitali yako?” aliuliza mama
“Anavyodai Tricia ni kwamba haiwezekani, lakini sidhani, au labda enzi hizi imebadilika, ila enzi zetu nakumbuka tulikuwa tunaenda popote” alisema mzee
“Mh...sawa”
“Sio vibaya, huko mbeya atakuwa chini ya uangalizi wa mdogo wangu, Isaac kwa hiyo sioni kama kuna shida inaweza kutokea”
Wakiwa wanaongea pale, Providence alishuka mapajani mwa baba yake, kisha akakimbilia jikoni ambapo alimkuta binti wa kazi ambaye pia alikuwa mgeni na sio yule Nusrat wa kipindi kile, huyu alifahamika kwa jina la Adela
“Daada” alisema Provi huku akijaribu kufungua jokofu (friji)
“Unataka nini wewe?” aliuliza Adela
“Nataka maji ya kunywa”
“Ngoja” Adela alisema huku akiacha kazi yake na kumfuata akamchukulia maji na glass kisha akachanganya ya kawaida na ya baridi ili asiumie kifua.
Providence alikunywa na kuondoka, na hata baadaye walipata chakula cha usiku na kulala.
*
Ugomvi kati ya mzee na mkewe ulishaisha muda mrefu, maana ilipofikia hatua mbaya, ilibidi mzee amueleze mkewe ukweli kuhusiana na mzee Salum Kaisi kutokuwa na uwezo wa kumpatia ujauzito, na hata walipopima DNA wakagundua kuwa Tricia ni binti yake wa kumzaa.
Mama Tricia aliomba msamaha na kusamehewa, maisha yakaendelea kwa furaha tu....
*
Usiku Tricia aliingia katika stand kuu ya mabasi jijini Mbeya. Kulikuwa giza totoro, lakini Frank alikuwa akimsubiri binti stendi.
Tricia alishuka kwenye gari huku akiwa anaongea na simu “Nimeshafika”
Frank akamjibu “Mbona niko hapa....tena nimeshakuona”
Tricia aliangaza akamuona kijana Frank akiwa amesimama kando kando ya gari yao, watu wanatiririka kutoka juu kwenye basi.
Bila uoga binti alimfuata akamkumbatia kwa nguvu “Wooow” alisema Tricia
“Woow...hongera kwa kufika salama”
“Asante....umekuwa mrefu” alisema binti huku akimuachia na kumtazama juu mpaka chini
“Yaani urefu mwezi huo mmoja tu ndo unasema nimekuwa mrefu?” alisema Frank wote wakacheka halafu binti akageuka ili kupokea mabegi yake yaliyokuwa kwenye buti la basi hilo.
Alipopokea waliondoka kwa pamoja kuelekea hotelini kwa ajili ya kupata chakula cha usiku “Mh ina maana hupikagi?” aliuliza Tricia huku akizidi kutembea
“Aaah, naona uvivu sana, lakini sio mbaya tutakula hapa kesho tutapika”
“Mh sawa” binti alisema huku akijikunyata na kusema “Ila huku kuna baridi”
“Haha...kawaida inabidi uwe na sweta...hapa sio Dar”
“Kweli nimeamini ile misemo ya baba kusema huku Mbeya kuna baridi”
“kwani hujawahi fika?”
“nilishafika ila kilikuwa ni kipindi cha kiangazi sio kama hiki”
“Oh sawa”
*
Frank na Tricia walikula halafu walichukua bajaji kuwapeleka alipokuwa amepanga Frank, palikuwa sio mbali sana, hata kwa mguu ilikuwa inawezekana kufika mjini, binti alifurahi kufika, kulikuwa sio kubaya, alioga kisha walipumzika.
Usiku ilikuwa ni purukushani, kupeana mahaba yasiyo ya nchii hii, mpaka ilipofika saa saba ndio walilala na tena asubuhi waliamshana na penzi zito la kutoana hang-over ya usiku.
Wakati wao wakifaidi viuno, kumbe kijana Maulid alikuwa kando ya bwawa la samaki, alikuwa anagombana na mchuuzi wa samaki, maana alikuwa ameacha biashara ya mkaa na kuhamia kwenye uvuvi ndani Ziwa Nyasa
“Haufanyi fresh broo....sasa hawa samaki tulivyowasotea hivi kweli unatupa elfu hamsini? Watu watatu tutagawana vipi”
“Maulid ee....samaki hawana soko,,,au kama vipi embu pelekeni wenyewe, maana lawama zimezidi” alisema mchuuzi wa zile samaki
“Fresh, haina noma mzee...bora tuende wenyewe” alisema Maulid kwa hasira
Yule jamaa aliondoka akawafuata wauzaji wengine, lakini Maulid na wenzake walibaki wakijadiliana wafanyaje, elfu hamisini kwa watu watatu waliona ni pesa ndogo sana kulingana na ugumu wa kazi waliyoifanya.
Baadaye wale wenzao walikubaliana wauze kwa bei hiyo hiyo, na waliuza wakampa shillingi elfu 20 halafu wao wakagawana shilini elfu kumi na tano kwa kila mmoja.
Maulid alienda mahali akajilza na kutazama angani, bado hakuona ndoto yoyote ikitimia, ni miaka mingi amekuwa akifanya kazi nyingi sana, tena kazi ngumu lakini kamwe hakufanikiwa kufanya kitu chochote cha maana, hakuwa na kiwanja, hakuwa hata na sehemu nzuri ya kujipumzisha kipindi akirudi mjini....JE NINI KITAFUATA? USIKOSE KIPENGELE CHA 02
KIPENGELE CHA 03
Samawati alikuwa ni mwanamke ambaye alimzoea sana Maulid, alikuwa ni mwanamke ambaye alikuwa na uchumi wa kati, maana alikuwa ni mtalaka wa mwanaume mmoja aitwaye Iddi Mponela ambaye mwanamke huyo alikuwa amezaa naye watoto wawili, lakini katika talaka waligawana watoto na kila mmoja akibaki na mtoto mmoja.
Jawabu ni mtoto wa pili wa Samawati, huku mtoto wa kwanza akiitwa Maulid kama ilivyokuwa kwa mwamba mvuvi, mkata mkaa ambaye ni Ex boyfriend wa Tricia. Na mtoto Maulid alikuwa akiishi kwa baba yake mzazi, maana kipindi akizaliwa yeye alikuwa na miaka kumi huku mdogo wake, Jawabu akiwa na miaka 4 na miezi kadhaa ikalazimika Samawati kuondoka naye.
Samawati alikuwa ni miongozi mwa wanunuzi w samaki katika eneo lile la ziwani wakati wavuvi wakishavua basi alinunua na kupeleka sokoni.
Maulid akiwa amejilaza chini ya mti huku akikumbuka maisha yake ya nyuma na jinsi alivyoshindwa kutimiza ndoto zake za kuwa wakili kutokana na kukosa ada, ghafla alisikia mtu kaketi kando yake halafu akavuta pumzi ya uchovu kwa nguvu
Maulid aligeuka na kumtazama, ni Samawati, “Ah sister” alisema Maulid na kugeuka akaendelea kutazama angani
“Nimechoka” Alisema Sama
“Pole” alisema Maulid
“Asante...vipi mbona umekaa hapa peke yako?” aliuliza Sama
“Ah nina mawazo yangu”
“Mawazo gani na wewe Maulid??” alisema halafu akakumbuka na kumuambia “Hivi unajua mwanangu mkubwa anaitwa Maulid
“Ah we....kwani una watoto wangapi?” aliuliza Maulid
“wawili”
“Wawili ulipata wapi wewe...kwanza una miaka mingapi?”
“Ah mimi nina miaka 35 unafikiri mimi mtoto kama wewe?” aliuliza
“Ahaaha....mimi nina miaka 31....sio mtoto”
“Ila kweli maana mimi nikiwa na miaka 31 nina watoto wangu wawili...,ndo utafute mke uoe sasa” alisema Sama huku akimfinya shavuni
“Daah...ila kweli” alisema Maulid na kuwaza mbaali...bado aliamini hana maisha ya kumfanya aweze kumtunza mwanamke, maisha yake ni ya kutegemea elfu hamsini kwa wiki, ni kipato kidogo kwa ajili ya matunzo ya familia, ukizingatia hakuwa na kiwanja, wala nyumba, hakuwa na godoro wala kitanda, alijikuta anarudi kwenye mawazo yake ya mwanzo, ambapo alijisahau na kutamka peke yake “Hivi nitaishi hivi hadi lini? Ina maana nitakufa masikini?” alijiuliza kwa sauti
“Khe...una mawazo....vipi tena mbona unaongea peke yako?” aliuliza binti
“Kosa kubwa ni mimi mwenyewe, nilikosea sana kuacha ile kazi ya kuuza mkaa, maisha yangekuwa marahisi” alisema Maulid
“Kwanini sasa uliacha?” aliuliza
Maulid alitikisa kichwa lakini akatabasamu maana alikumbuka chanzo chake kuachana na ile kazi, ni kwa sababu alikuwa amemkosa tu mwanamke ambaye alikuwa amempenda kwa muda mrefu sana.
Maulid alijicheka na kumtazama Samawati halafu akasema “Ni boss tu alinizingua na pesa yangu”
“Hahaa...pole ila nili....” kabla Samawati hajamalizia sentensi ndipo akasikia anitwa, na aligeuka akakuta kuna kijana alikuwa akimuita, mwanamke akasema “Nini???”
Yule kijana akamjibu “Usafiri unaondoka twenzetu”
Samawati alishtuka na kuinuka akasema “Khe, kumbe gari imeshafika, twende mjini”
“Wapi?” aliuliza
“Ah,....mh nataka nielekee Mbeya mjini nataka nikamuone mwanangu maana anaumwa sana”
“Anaumwa?” alisema Maulid huku akiinuka na kuvaa tisheti
“Ndio,....twende mjini” alisema mwanamke huyo
“Nauli ya usafiri shilingi ngapi?”
“We twende nauli hamna....”
“Mh sawa”
Maulid alijikuta amechotwa bila kutarajia, na kuelekea kwenye gari, wakapanda na mizigo ya samaki wakaelekea sokoni.
Baaadaye mida ya saa 09 jioni, Maulid na Tricia walikuwa mjini, walikuwa wakitembea kutoka katika stendi ya nane nane kwenda kwenye hoteli moja ili wakapate kwanza chakula kabla hawajaenda kumuona mtoto Maulid ambaye alikuwa anaumwa.
Waliingia katikati ya hoteli moja na kuketi.... Samawati akamuuliza “Utakula nini?”
“Nataka ugali nyama” alisema Maulid
“Okay....mi nipatiee......spaghetti naaa.....kuku” alisema mwanamke huyo.
Sio kwamba Maulid hakutamani kula vizuri zaidi lakini alihofia pesa yake mfukoni, maana alihisi atalipa mwenyewe.....waliletewa juisi kwanza, halafu story ziliendelea
“Maulid, nikuambie kitu? Licha ya maisha magumu ipo siku utakuwa safi....mi nikueleze tu”
“Anhahaa...nawaza hapa nirudi kwenye biashara ya mkaa....yaani nikiwapata wanangu, kazi inaendelea” alisema
“Namba zao huna?”
“Nilitupa simu....ila ninajua pa kuwapata”
“Daaah....unajua nini? Nikuambie kitu?” alisema Samawati
“Niambie”
“Ninahitaji kupata mtoto wa kike....mi nitamtunza peke yangu....unaweza kunisaidia?” aliuliza Samawati huku akimtazama Maulid kwa uso mkavu uso na aibu
Ilibidi Maulid atabasamu kwanza huku akifikiria ni jibu gani ampatie....
Wakati akifikiria cha kumjibu, kumbe nje ya hoteli ile waliyokuwa, ndipo pia alipokuwa amesimama Tricia pamoja na Frank ambaye ni mpenzi wake mpya huku wakiulizana
Frank: Tuingie hapa kuna juisi nzuri tu mbona?
Tricia: Mh ni patulivu?
Frank: Twende ukapaone, usipopapenda si tunatoka? (Frank aliongea huku akimshika mkono na kujaribu kumvuta ili waingie ndani, ambapo kule kule ndani kulikuwa na Maulid pamoja na Samawati wakiwa wanapata chakula kwa pamoja)
Tricia alikubali kupiga hatua ili aongozane aingie ndani pamoja na Frank.
JE UNAHISI TRICIA AKIONANA NA MAU PALE NDANI ITAKUWAJE? USIKOSE KIPENGELE CHA 3
KIPENGELE CHA 03
Tulipoishia
Frank: Tuingie hapa kuna juisi nzuri tu mbona?
Tricia: Mh ni patulivu?
Frank: Twende ukapaone, usipopapenda si tunatoka? (Frank aliongea huku akimshika mkono na kujaribu kumvuta ili waingie ndani, ambapo kule kule ndani kulikuwa na Maulid pamoja na Samawati wakiwa wanapata chakula kwa pamoja)
Tricia alikubali kupiga hatua ili aongozane aingie ndani pamoja na Frank.
Endelea
Maulid na Samawati walikuwa wanatazamana, huku Maulid bado akitoa tabasamu
“Mbona hujanijibu?” aliuliza Sama
“Haha...unazingua Samawati” alisema Maulid na kuendelea kula ugali
“Haki ya Mungu....nina hamu kweli ya kupata mtoto wa kike....wa mwisho kisha niachane na suala la kuzaa” alisema Samawati
“Seriously?” Maulid aliuliza
Sio kwamba Maulid alikuwa hataki, ila alihisi Sama anamtania kwa sababu alikuwa hana mahusiano naye, wala hawajawahi kutongozana katika maisha yao yote.
Wakati wakiulizana ulizana pale, ndipo Tricia na Frank walifika ndani ya hoteli, kwa bahati nzuri au mbaya, katika meza aliyokuwa amekaa Maulid alikuwa ameupa mgongo mlango wa hoteli, hivyo hata alipoingia Tricia na Frank wala hakuweza kuwaona.
Kulikuwa na watu wengi pale hotelini, Tricia aliona aibu na kutoka nje baada ya macho kama 30 hivi kumtazama kwa wakati mmoja.
Frank akamfuata na kumuuliza “Vipi mbona umeondoka tena?”
“Ah....mimi bhana, watu wengi, embu tutafute sehemu nyingine” alisema binti
“Ah,,...yaani wewe unazingua kichizi” alisema Frank kwa hasira na kumfuata, walipofika nje walitembea tembea kwa mwendo wa taratibu, ndipo Frank akasema “Kitandani mbona huonagi aibu”
“Hahahaaaaa......” binti alicheka kwa nguvu, kicheko ambacho kilisikika umbali mrefu kidogo kikatembea mpaka kikapenya ndani ya hoteli na kuingia kwenye masikio ya Maulid.
Ni muda mrefu ulikuwa umepita tangu Maulid alipoachana na Tricia jijini Dar es salaam...lakini kamwe ubongo wake haukuweza kusahau namna binti alivyokuwa akicheka. Alihisi kitu na alibaki anashangaa lakini alijitia moyo kwa kuwaza kwamba binti sio rahisi akawa mjini Mbeya.
“Duh” alisema Samawati
“Vipi?? Nambie” Maulid
“Mbona kama unawaza mbali?”
“Hamna...ila ni kwamba mimi nawaza unanitania ulichokisema, unataka mtoto wa kike, sasa mimi ninakusaidiaje?” aliuliza Maulid huku akili yake ikiwa bado kwenye kile kicheko cha Tricia ambaye alikuwa ameshaondoka muda mrefu
“Sasa wewe si mwanaume na mimi mwanamke? Mi ninahitaji kuzaa na wewe...naomba...mi sihitaji kuolewa nahitaji mtoto mwingine wa mwisho...nipatie mimba Maulid”
Maulid alimtazama, kweli yule mwanamke alionesha kwamba anamaanisha kile alichokuwa anakisema hivyo Maulid akaanza kumuamini na kumuuliza “Je asipokuwa wa kike?”
“Ah...basi tu nitamshukuru Mungu, ila mimi natamani kuwa na binti”
“Sawa, basi tutaongea” alisema
“Poa andika namba yangu halafu utanitumia ujumbe niijue ya kwako”
Maulid alitoa simu mfukoni, halafu akaandika namba ya Samawati, na kumtumia ujumbe.
Lilikuwa ni bingo, Maulid bado hakuwa na mtoto hata mmoja, alihitaji kuwa na mtoto maana umri umeshaenda. Kichwani alifurahia wazo la Samawati kuhusiana na kumpatia mtoto wa kike, alijiona anaenda kuitwa baba lakini hatomtumikia huyo mtoto, kwa hiyo hiyo ndiyo furaha yake.
BAADA YA WIKI MOJA
Ilikuwa ni siku ya jumapili asubuhi, Maulid alimka mapema sana na kwenda kupanda gari kuelekea Iringa, kule alikuwa anaenda kuangalia kama atawapata wale marafiki zake, kina Johnson na Musa ambao alikuwa akifanya nao kazi.
Aliamini atawapata iringa kwa sbabu yale ndiyo yalikuwa masikani yao licha ya kufanya zaidi kazi wakiwa mkoani njombe.
Maulid alijua hata kama asipowapata basi atapata namba zao kwa urahisi zaidi, ili aweze kuwasiliana nao.
Alikuwa akiwaza mambo mengi sana Maulid, na alikumbuka mara ya mwisho akiwa jijini Dar es salaam baada ya kutoka katika kituo cha polisi, askari mmoja alimfuata akamuambia “Samahani anataka kuongea na wewe”
Maulid akamuuliza “Nani?”
“Dr Mwaipopo”
“Ok”
Maulid kipindi hicho alipokeaga simu halafu akaongea “Hallo”
Mzee akasema, “Sasa sikiliza, mimi baba yake Tricia....ninakuomba kitu kimoja”
“Kitu gani?”
“Binti yangu sitaki afeli....nachoona kwake kama umemloga sijui mwanangu maana nyie mnakuwaga na majini sana....sikiliza, nenda kakae na mwanangu umtie moyo asome. Halafu akishamaliza mitihani yake, sitaki kukuona ukiwa na ukaribu naye”
“Mzee siwezi” alisema Maulid
“Hauwezi...sio kwamba sipendi muwe karibu ila nina mikakati yangu...kafanye hivyo mimi nitakupa milioni moja, uondoke ukaanzishe maisha yako huko mbele ya safari....”
Hili suala la milioni moja lilimchanganya mtaalam na kujikuta anakubali kuwa karibu na Tricia na kila siku alikuwa anamuambia asome kwa bidii asije akafeli somo lolote. Hii ilisaidia ila cha kushangaza, baada ya binti kumaliza mitihani, mzee Mwaipopo hakumpa Maulid milioni kama alivyokuwa amemuahidi, Maulid aliumia sana sana sana....alimtafuta mara kwa mara mzee lakini mzee akawa anamjibu karaha.
Hii ilikuwa ni kumbukumbu aliyoikumbuka Maulid, lakini iliishia pale alipofika kituo cha mabasi, alishuka kwenye gari halafu akaanza kutembea kuutafuta mtaa ambao aliamini atawakuta kina Johnson pamoja na Musa, ili wampe dili lingine la kufanya kazi.
Maulid aliingia chocho ya kwanza na ya pili, ndipo akaanza kukutana na watu wanaomfahamu wakaanza kumshangaa
“Zabuniiii....kheee upo??” mama lishe mmoja alimuuliza huku akimshangaa, kana kwamba ameona kitu cha tofauti kabisa
“Nipo bi mkubwa, shikamoo” alisema Maulid huku akipita
“Marahaba” aliitika yule mama huku akiwa ameshika kiuno anamshangaa....
Maulid hakuelewa kwanini anamshangaa....alizidi kutembea, kila alipopita watu walimchangamkia sana na hata alipofka mtaa Msikitini, aliangukia katika kijiwe kimoja akakuta boda boda kadhaa.
“Yule sio mau?” aliuliza boda boda moja, washikaji wote wakaangalia, ni Maulid kweli
“Jesus....” alisema kwa mshangao kijana mwingine
Maulid aliwafikia
“Oya vipi?” aliuliza
“Maulid” alisema kijana mmoja akiwa anamshangaa
“Vipi mbona nakatiza kila chocho watu wananishangaa?” aliuliza
“Ni wewe?” aliuliza kijana huyo ila ghafla Maulid alipokea simu kutoka kwa Samawati.
“Hallo” alisema Maulid
“Uko wapi Maulid...?”
“Niko iringa?”
“Iringa? Mbona mbali....mi nilijua upo karibu tuonane”
“Vipi tena kuna shida?”
“Ndio....kama unaweza kuja Mbeya leo, njoo si unakumbuka mpango wetu”
Maulid kusikia vile, alisikia ameshtuka moyo paah....alitakiwa akampe mimba yule mwanamke kama walivyokubaliana, na katika kupeana mimba kuna tendo linatakiwa lifanyike ambalo ni tamu zaidi, hivyo alimjibu haraka
“Narudi Mbeya leo leo, si utakuwepo?”
“Nitakuwepo nakusubiri wewe”
“Haya poa”
Maulid alikata simu kisha akamfuata bodaboda mmoja
“Mwanangu nina haraka, ila nimekuja kuwatafuta wanangu Johnson na Musa, vipi wapo huku au mnipe namba zao?”
“Johnson...???? Musaa??” aliuliza Bodaboda
“Vipi mbona unauliza kwa mshangao”
“Maulid? Embu acha mambo yako. Kwani ulikuwa wapi wewe miaka miwili yote? Sisi wanao hatukujua upo hai”
“Nipo mwanangu, nilijichimbia mbali ila, kiukweli niliimiss sana hii mitaa”
“Daah...kwa hiyo hujui lolote kuhusu Johnson na Musa?” aliuliza
“Sifahamu kwani kuna nini man?” aliuliza kwa mshangao mkubwa
“Mzee,....sisi wenyewe tulishangaa kukuona, tulijua labda ulikuwa nao...mbona walipata ajali Makambako wakafa aisee...muda mrefu sana?” aliuliza kijana huyo
“Wamekufa????” aliuliza kwa mshangao Maulid.....ITAENDELEA

Nzur sana
ReplyDelete