FURAHA YANGU ILIPO SEASON 2 EPISODES 19 - 21 FINAL

 


FURAHA YANGU ILIPO
SEASON TWO 19 HADI 21 (MWISHO)

Na Mr AB ENTMENT

KIPENGELE CHA 19
Tricia alipitia wakati mgumu kuelewa afanye nini, hii ni baada ya kuchukua vipimo na kugundua kuwa ana ujauzito wa mwezi mmoja na wiki moja. Alitabasamu na kujiuliza “Hivi mimi nina wazimu?” halafu akashika tama na kuwaza “Ninataka mzee Mwaipopo aniue?” yalikuwa ni mawazo mengi sana juu yake.

Alifikia hatua akaona kuliko kupoteza ukaribu na baba yake ni kheri akaitoa ile mimba japo mwanzo alikuwa anatamani kumzalia Maulid.

Kabla hajachukua hatua ya kutoa mimba, binti alimtumia ujumbe Maulid “Baby I am sorry acha tu nitoe hii mimba” alipoituma ile message alisubiri majibu yalirudi baada ya dakika nane

Maulid alituma ujumbe unasema “Mimi hapa nina miaka 31 tena inaelekea 32, naomba usiitoe hiyo mimba natamani kuitwa baba, na sio baba kwa mtoto aliyetokana na mtu mwingine bali awe ametoka kwako mpenzi, naomba please”

Tricia aliusoma ule ujumbe ulibeba hisia za Maulid, alikuwa anampenda lakini sasa hata kama anampenda je Maulid ana uwezo wa kuilea familia ilhali hata kujilea mwenyewe ni changamoto?

Binti akamtumia ujumbe “Maulid...baba angu akijua atanitelekeza moja kwa moja”

Maulid akajibu “Hata akikutelekeza tutaishi wote...mi nataka nikuoe”

“Haha...utanioa tutakula nini? Maulid sikiliza bwana mi natoa”

Kwa upole Maulid alijibu “Sawa Tricia kama utaamua kuitoa mimba yangu nitashukuru pia...mi sina bahati ya kuitwa baba” 

Binti alipata majonzi mazito na kujikuta anaumia sana, alijuta kuishika mimba, alifikiria mambo mengi, naye pia umri umeshafika miaka 26 kasoro, ni umri sahihi wa kupata mtoto lakini ndio hivyo bado ni tegemezi kwa baba yake, na vile vile baba yake alikuwa ni mkali na mwenye misimamo mikali, sasa alijua kwamba baba hatoafiki kabisa katika suala la binti kushika mimba bila kuwa na ndoa.

Tricia alizidi kuumiza kichwa, ndipo baadaye akapata ushauri kutoka kwa mama mdogo (mke wa Isaac) akamuambia kwamba ampigie simu baba yake amuombe pesa ya kufanya biashara halafu akishaanza biashara zake atamuambia baadaye kwamba ana mimba.

Ili lilikuwa ni wazo lililobeba nafasi katika moyo wa binti na hata kujikuta anaafiki.
Alimfuata baba mdogo Isaac na kumuomba ushauri kwamba pale Mbeya afanye biashara gani nyepesi ambayo haitamzuia kufanya mambo mengine, akapewa ushauri nasaha

Jioni alimpigia simu baba yake
MZEE MWAIPOPO: Hujambo mwanangu?
TRICIA: sijambo daddy, nyie mnaendeleaje?
MZEE MWAIPOPO: tuko salama, Mungu ni mwema
TRICIA: anhaa...nimepamiss sana nyumbani
MZEE MWAIPOPO: ujue sasa
TRICIA: nitakuja baba...ila uliniambia kwamba niangalie wazo la kufungua biashara kisha nikuambie
MZEE MWAIPOPO: anhaa...umepata wazo la biashara gani?
TRICIA: Ah...nimekaa na Ba mdogo akanishauri hapa mjini biashara ya stationery, pamoja na miamala ya simu inaweza kuwa biashara nzuri sana nikapata hela nyingi
MZEE MWAIPOPO: Kweli nafikiri ni wazo zuri....amekueleza kwamba inaweza kugharimu shilingi ngapi?
TRICIA: Kwa hiyo ya stationery tu...ni milioni kumi halafu hiyo nyingine labda itaanza baadaye maana mh pesa ni nyingi baba
MZEE MWAIPOPO: anhaa ni kweli ila ni wazo zuri...nafikiri nipe nafasi nitalifikiria hili halafu nitakupa taarifa...kwa hiyo Dar hutaki kuja tena?
TRICIA: si ndo mpaka nimalize baba?
MZEE MWAIPOPO: sawa...basi sawa nitaliweka kichwani kisha tutamalizana, nitakutumia, fuatilia na hiyo ya mambo ya pesa. Labda inaweza ukaanza zote kwa pamoja
TRICIA: sawa baba, kwa hiyo nikutafute lini?
MZEE MWAIPOPO: nafikiri ufanye mwishoni mwa mwezi, ili nijue bajeti inaendaje, si unajua mimi sina mamlaka na pesa pale hospitalini anayenilipa ni muhasibu wangu, yaani utafikiri pesa sio ya kwangu
TRICIA: hahahaaa 
MZEE MWAIPOPO: unacheka ee?? (mzee alitabasamu)
TRICIA: ndio...halafu nimemiss kuendesha gari...sijui nije
MZEE MWAIPOPO: hahaa....mama yako ndo analifaidi sasa
TRICIA: haya nitampigia nimsalimie baba

Tricia aliagana na baba yake, na baba hakuelewa lengo la binti ni nini.....ITAENDELEA

KIPENGELE CHA 20
Mwisho wa mwezi ulifika, kama ilivyo kawaida kwa mzee Mwaipopo hakusita kutuma kiasi cha pesa kilichohitajika kwa ajili ya biashara ya binti yake. Alikuwa anampenda sana na hakutaka binti apitie mateso kabisa.

Tricia akiwa kifuani mwa Maulid alimuambia “Baby kwanini hii project usiisimamie wewe?” aliuliza

“Niisimamie mimi?? Sasa mi na masuala ya stationery wapi na wapi?”

“Baby hamna kitu kigumu kwenye stationery, ukishajifunza wiki moja tu unakuwa sawa....”

“Mh...haya sawa”

*
Mipango iliendelea binti alifungua bonge la ofisi, baada ya miezi mitatu aliongeza miamala kama alivyokuwa ameahidi.
Ilifanya vizuri kwani biashara inazidi kuwa nzuri kulingana na mtaji mzuri uliokuwa umetumika kuianzisha.

Maulid alisimamia biashara, lakini vile vile mimba ya Tricia ilikuwa ni kubwa tayari tumbo lilionekana, Frank aliumia sana kuona bado wawili wale wanapendana kisawasawa.

Walimuweka binti mmoja awe ndo anafanya kazi stationery ila Maulid alishughulika na miamala tu.

*
Siku moja mzee Mwaipopo, aliamua kwenda Mbeya kutembelea ndugu zake, mzee Mwaipopo pia alihitaji kuonana na binti yake, lakini hakumtaarifu kwamba atafika Mbeya hivyo alifanya kama surprise.

Usiku mke wa Isaac alichukua simu na kumtumia ujumbe Tricia
“Vipi T hivi baba yako anajua una mimba?”

Tricia akajibu “Hapana hajui....kwani vipi?”

“Jiandae kisaikolojia baba yako amekuja Mbeya leo”

“Amekuja Mbeya???” aliuliza mtoto wa kike kwa kuchanganyikiwa kwani hakutamani baba amuone katika ile hali, halafu mbaya zaidi alikuwa na mimba ya mtu ambaye anajua kabisa baba yake alikuwa hampendi hata kidogo....aliogopa

“Ndiyo yupo Mbeya”

“Amefuata nini??”aliuliza Tricia

“Kaja eti kusalimia na kukuona pia, ameamua kukufanyia surprise” alisema mke wa Isaac kisha akamtumia mumewe message “USIMUAMBIE KWAMBA TRICIA ANA MIMBA”

Isaac aliisoma kimya kimya na kukausha.

Huku kwa Tricia alimuita Maulid “Baby”

“nini mbona kwa mshtuko?”

“Baba yuko Mbeya, inabidi kesho usifungue...uwiii itakuwaje kuhusu hili tumbo jamani??” alichanganyikiwa mtoto wa kike hakujua afanye nini maana mimba ni kubwa na hakutak baba aione, alitamani asikie tu ana mjukuu.

Mawazo tele yalikuwa upande wa mtoto wa kike, usiku wala hakulala.....na asubuhi ilipofika Maulid aliamua kumtorosha na kumpeleka kule Kyela alipokuwa akiishi kipindi cha nyuma hii ni kumuepusha na baba yake kabisa.

Dr Mwaipopo aliamka akampigia binti yake simu kwani inapatikana? Tafuta mpaka akachoka binti hapatikani kabisa. akamuuliza Isaac

“Vipi mbona Tricia hapatikani?”

“Ah...mh sijui” alisema Isaac

“ah...au atakuwa hospitalini?”

“Huenda...ila cha muhimu twende kwanza pale kwenye ofisi yake tunaweza kupata taarifa kamili”

“Sawa”

Mzee Mwaipopo hakuwa na wasiwasi kwa binti yake, alikuwa anamuamini kabisa, aliamini ataonana naye, alijua binti yake anampenda sana, na ni kweli walipendana lakini ndio hivyo binti alishaamua kukaa kando na kuangalia kwanza mapenzi yake

Isaac na baba Tricia waliondoka nyumbani saa tatu asubuhi, wakaenda na gari ya Isaac mpaka pale kwenye stationery ya binti wakakuta pamefungwa bado
“Mh hajafungua bado” alisema Isaac

“Sasa saa tatu hii biashara haijafunguliwa hayuko serious” mzee Mwaipopo alisema kwa hasira alikuwa anjua time is money, hakupenda muda upotezwe kabisa.
Alitazama bango la kuitangaza steshenari limeandikwa TRICIA STATIONERY akatabasmu kidogo na kusema “Watoto wa kike wana mbwembwe”

“Mi naona tuende kwake tunaweza kumkuta au tuende hospitali??” aliuliza binti

“Wapi?”

“Hajapanga mbali...twende ninapajua maana mimi ndiye nilimpelekea vitu”

“Sawa”

Walipanda gari na safari ilianza, ila walipofika wakakuta mtu hayupo....wakaamua kwenda hospitali lakini napo pia walimkosa.

Mzee Mwaipopo alishangaa sana, hakujua binti yake yuko wapi, kila akimtafuta kwenye simu binti hapatikani.

Ghafla akiwa anawaza, mzee alipokea ujumbe kwenye simu yake, akaufungua ulitoka kwenye namba mpya na ulisema hivi
“DADDY....NIKO NJIANI NINAKUJA DAR”

Mzee Mwaipopo alishtuka sana na kumuuliza Isaac “Huyu mtoto ni kichaa....aliwaambia anaenda Dar?”

“Dar????” Isaac aliuliza kwa mshangao

“Ndio”

“Hapana”

“Embu soma hii message yake” alisema mzee huku akimpa simu Isaac

Wote walishangaa hakuna aliyekuwa na taarifa hiyo, na wala haijulikani hilo wazo binti alilipata wapi.
Mzee alipojaribu kupiga simu binti ameshazima siku mingi anabembelezana tu na Maulid.

Mzee Mwaipopo alipata wakati mgumu, lakini alishukuru aliona binti yake amejiongeza na kufungua biashara.
Usiku Mzee alimpigia mke wake akamuuliza kuhusu binti kufika nyumbani cha kushangaza sasa mama alijibu
“AMESHAFIKA NA KULALA, AMECHOKA NA SIMU AMEPOTEZA”
JE HII INATOKEAJE? EMBU TUSIKOSE KIPENGELE CHA 21

KIPENGELE CHA 21
Mzee Mwaipopo hakujali aliamini ni kweli binti alikuwa ameenda nyumbani kwenda kuwasalimia lakini hii ilikuwa sio kweli...ni kwamba Tricia alipoona maji yamemfika shingoni, aliamua kumtafuta mama yake na kumpanga kwa kutumia simu ya mtu mwingine

Mazungumzo yalikuwa hivi
“Mama...mwenzako nina shida na sijui utanisaidiaje”

“Shida gani tena Tricia?” aliuliza mama

“Niahidi kwamba utanisaidia”

“Kama nina uwezo nitakusaidia” mama T alisema

“Mama...baba kaja Mbeya...nimemkimbia...sitaki anione”

“Kwanini hutaki kumuona baba yako?”

“Mama bhana mimi nina mimba ya miezi mitano...baba ni mkali eti”

“Tricia...una mimba?????” mama aliuliza kwa mshangao

“Ndio mama”

“Ya nani??”

“Ni ya kijana mmoja tulikutana huku Mbeya tukaingia kwenye mahusiano na likatokea hilo”

“Tricia, hivi uko serious na maisha?? Yaani unashika mimba hata kazi hujapata?? Hujamaliza hata shule?? Unadanganywa na hizo laki tano unazolipwa ee?? Tricia umepote mwanangu...umepotea”

“Mama naomba unisaidie...”

“Sina cha kukusaidia, tena ninamuambia sasa hivi mpumbavu mkubwa wewe” mama alisema kwa hasira kisha akakata simu

Tricia akamtumia ujumbe wa haraka “NIMEMUAMBIA BABA KWA NIPO DAR, NAOMBA AKIKUULIZA MWAMBIE NIPO DAR UTAKUWA UMENISAIDIA, MI NITAMUAMBIA SIKU NYINGINE ILA SIO ANA KWA ANA MAMA ATANICHUKIA SANA”

Mama Tricia baada ya kuona ule ujumbe alijikuta moyo umelainika, licha ya kwamba aliumizwa na kitendo binti alichokifanya lakini hakuwa na namna, ilibidi amsaidie ili asichukiwe na baba yake.

Mzee Mwaipopo kesho yake, alipanda ndege na kurejea jijini Dar es Salaam, alijua atamkuta binti yake lakini wapi.

Tricia naye alipopewa taarifa na mama mdogo kwamba baba ameondoka, basi aliamua kurejea jijini Mbeya na kuendelea na kazi zake za kila siku.

Alimtumia ujumbe baba yake
“DADDY I AM SORRY”

Baba akauliza “SORRY FOR WHAT??” 

Binti akajibu “I AM PREGNANT” alisema kwamba ana mimba

“PREGNANT? PREGNANT FOR WHO??” aliuliza baba kwamba una mimba, mima ni ya nani??

“NISAMEHE BABA, NIMEBEBA MIMBA YA MAULID”

“MAULID GANI??”

“YULE KIJANA WA KIPINDI KILE”

Mzee Mwaipopo alipatwa na hasira za kufa mtu, akachukua simu na kumpigia binti akamkatia, hataki kuongea naye ana kwa ana.

Mzee akamletea noma sana mkewe kwa kujua ndiye anacheza trick za kipumbavu na mtoto.

Alimtumia ujumbe wa mwisho
“NIKUAMBIE KITU KAMA UMEBEBA MIMBA BILA KUINGIA KWENYE NDOA, TENA MIMBA YA HUYO MPUMBAVU, NAOMBA TUSIJUANE MIMI NA WEWE...NIMEKUSOMESHA KWA GHARAMA NIMEKUPA PESA ZA BIASHARA KUMBE NDIO USHENZI UNAFANYA MJINGA WEWE? KUANZIA LEO MIMI SIKUTAMBUI KAMA MWANANGU, ENDELEA NA MAISHA YAKO NA HUYO MPUMBAVU MWENZIO”

Mzee alikuwa na hasira kweli kweli...hakujua afanye nini, aliona binti hana akili hata kidogo alikasirika sana.

Tricia alimtumia ujumbe “NDIYO MAANA NIMEOMBA MSAMAHA, KAMA UTANISAMEHE SAWA, KAMA HAUTANISAMEHE BASI HAMNA TATIZO, LABDA TUTAONANA TENA BABA...THANK YOU FOR EVERYTHING, I LOVE YOU”
Huu ujumbe binti aliandika akiwa anatokwa na machozi maana alishapitia mambo mengi sana yeye na baba yake, alimpenda sana baba na hakutarajia kama ipo siku watatenganishwa na kosa kama hilo. 

Alijitia moyo, huenda akishazaa mtoto basi baba atampenda tena kama ilivyokuwa mwanzo. Kikubwa ni kwamba baba alikuwa ameshampatia pesa ya mtaji na elimu, vyote hivi binti alipaswa kuvitumia kwa ajili ya maendeleo yake binafsi bila kumtegemea mtu

Ukaribu wake uligeukia kwa Maulid, Maulid alikuwa sio mwanaume mkorofi, waliishi pamoja licha ya kutokuwa na ndoa, walifanya kazi kwa pamoja,

Ukaribu ulihamia pia kwa baba mdogo, mara nyingi akiwa na matatizo, alikuwa akimfuata baba yake mdogo (Isaac) na kupata msaada.

Hivi ndivyo binti aliaga maisha ya kuishi na baba, akaamua kufuata penzi la mwanaume wa ndoto kuliko la wazazi wake wenye pesa nyingi.

Baada ya miezi minne binti alijifungua mtoto wa kiume na kuanza kuitwa mama hata leo....lakini ana ndoto kwamba ipo siku mapenzi ya baba yatarudi tena kwani maumivu huwa yanapita

THANK YOU FOR BEING WITH ME IN THIS STORY

HAPA NDIO MWISHO WA HADITHI HII....HAITAENDELEA TENA

Imeandikwa na Mr AB Entertainment

WhatsApp number 0743433005 (TANZANIA)
FACEBOOK: STORY ZA MR AB
Karibuni kuna hadithi nyingine nyingi....BYEEE

4 Comments

Previous Post Next Post