FURAHA YANGU ILIPO
SEASON TWO 07 HADI 09
Na Mr AB
KIPENGELE CHA 07
TULIPOISHIA
Wakati anamlisha Tricia na Frank waliingia pale ndani ya hoteli, binti akashuhudia live Samawati akamepelekea nyama na kijiko mdomoni mtaalam Maulid.
Alishtuka akamtazama, anahisi anamfananisha lakini ilikuwa hii ni kweli...binti aliduwaa na kujikuta ameganda kama kapigwa na shoti akawa anamshangaa Maulid.
Lakini Maulid alikuwa hajamuona binti maana macho aliyaelekeza kwa Samawati kabisa
ENDELEA HAPA
“Vipiii” Frank aliuliza kwa hasira baada ya kumuona binti ameganga anashangaa sehemu moja, ikabidi naye aelekeze macho kule binti alipokuwa anaangalia ndio akagundua kuna watu wanapeana mahaba hotelini kulishana lishana vyakula.
Frank hakugundua kuwa yule ni Maulid maana alikuwa hamjui kabla, alimshika mkono binti na kumvuta akamuambia “Twende bwana mi nachelewa hospitali ujue”
“Frank....” binti alisema
“Nini?”
“Tuondoke hapa” alisema binti
“Kwanini sasa?” aliuliza mtaalam
“We tuondoke”
“Ok”
Frank alitoka kwa hasira na kuondoka moja kwa moja kuelekea hospitalini, alimuacha Tricia akiwa amesimama nje ya hoteli
“It’s him” alisema kwamba ni yeye “How comes....mbona yuko huku?” alijiuliza binti huku akitaka kurudi ndani ila akaogopa na kusema “Nitakuwa nimemfananisha, sio yeye” alijisemea na kwenda kuchungulia ndo kabisa Samawati alikuwa anachezea ndevu za jamaa yaani kwa kifupi Sama alikuwa ameshampenda Maulid bila kutarajia.
Yaani binti alishtuka kiasi kwamba aliweka mikono mdomoni kushangaa....aliondoka haraka, hakutaka Maulid amuone kwa mara ile.
Tricia alipanda bajaj mpaka nyumbani, moyo wake wote ulikuwa umejawa na simanzi, yaani hakutarajia kumuona Maulid, halafu kilichomuuma zaidi ni kwamba alikutana na Maulid wakati Maulid alikuwa ameshaingia kwenye mahusiano na mwanamke mwingine
Alikumbuka siku ile alipokuta simu ya mwanamke yule, ni kwamba kuna namba ilimpigia na kumbuka alikuwa ameipigia Maulid, akaona jina limehifadhiwa Maulid, ndio sasa akaanza kupata picha
“Kumbe yule aliyempigia simu alikuwa ni Maulid jamani” alijisemea “Ina maana yule atakuwa ndio mwanamke wake?” alijiuliza swali “Ah kwanza hata akiwa na mwanamke mi si nina mwanaume wangu pia?” binti aliendelea kuwaza mambo mengi
Kiukweli licha ya kuishi bila kuwa pamoja kwa muda mrefu sana, bado Maulid aliishi akilini mwa Tricia hii ni kwa sababu ni mwanaume ambaye alimfungulia ulimwengu wa mapenzi.
Kilichokuwa kinamfanya aishi moyoni mwake, ni kwamba Maulid na Tricia hawakutengana kwa ugomvi wao, ila baba ndiye alikuwa hamtaki Maulid kwa sababu ya dini na pia kwa sababu alikuwa ni ndugu wa watu waliowahi kumnyima mke ambaye alikuwa anampenda enzi za ujana wake.
Wakati binti akiendelea kuwaza mara simu yake iliita kwa mtetemo, akaitoa kwenye pochi, ni namba mpya, akapokea na kusikilizia sauti
“Hallo...habari Tricia” alisema mwanamke aliyekuwa amempigia simu Tricia
“Salama” binti alijibu kwa mkato huku akiwa anasikilizia sauti kama anaifahamu au la
“Ah...samahani mimi mama Maulid ambaye uliniambia nikuletee samaki pale hospitalini jana”
“Ohhh....dada shikamoo” alisema binti kwa uchangamfu baada ya kujua kuwa ni Samawati alikuwa amempigia
“Marahaba mambo?”
“Poa tu...nambie dada angu” alisema binti licha ya kuwa na wazo tofauti kwani alikuwa ashamrithi ex wake
“Kuna rafiki yangu kaja mjini na mboga....vipi nikuletee?” aliuliza
“Samaki you mean.....right??”
“Ndio”
“Naomba niletee...ni shillingi ngapi vile?”
“Elfu kumi,....ni wakubwa”
“Okay niletee” alisema“Kwanza unaishi wapi wewe?” aliuliza Sama
“Mi naishi hapa Itua, ukifika tu centre hapa nakuona”
“Okay”
“Sawa” alisema binti lakini kabla Samawati hajakata simu ikabidi Tricia amuite “Dada samahani”
“Bila samahani...”
“Eti.....” alitaka kumuuliza swali lakini akaogopa “Au basi”
“Niambie tu mdogo wangu”
“Hamna...basi we niletee....kwanza unakuja mwenyewe?” aliuliza
“Nimefuatana na mtu...kwani kuna tatizo?”
“Hapana”
Tricia alikuwa ashaanza kuhamisha akili yake, alikuwa anamuwaza tu Maulid, hakujua Maulid alimpaga nini kipindi walipokuwa kwenye mahusiano, Tricia alipomuona mara ya pili alijikuta anaumia sana sana sana lakini akajitahidi kuficha maumivu yake akiamini ana maisha mengine kwa sababu alikuwa na mwanaume mwingine ambayee ni Frank Bukuku.
Basi, ilipita kama dakika arobaini na tano ndipo binti alisikia simu yake imeita akapokea
“tumeshafika hapa Itua uko tunakusubiri”
“Mh mbona chap hivyo....mlikuwa na usafiri gani?” alisema binti huku akishuka kitandani na kuanza kutoka nje ya chumba
“Nilikuwa na dereva ...mmoja hapa ana fujo kweli kweli” alisema Sama kwa utani
“Ahaha...nakuja hapo sasa hivi”
“Sawa”
Tricia alienda na mawili kichwani, alitamani kuonana na Maulid na alitamani vile vile kupata samaki akapike maana ni muda sana alikuwa amemiss, alifungua geti na kutoka barabarani
Kulikuwa sio mbali yaani alisimama nje ya geti akamuona yule mwanamke amesimama karibu na kijiwe cha boda boda japo sio rahisi kumuona lakini muda huo, dereva ambaye alikuwa ni Maulid alikuwa anashindana na vijana wa pale itua kupiga norinda na pikipiki ambayo hata sio ya kwake. Alipenda sana ujinga, vijana walimzoea kwa haraka
Samawati alimuacha akicheza na pikipiki, yeye akamfuata Tricia kwa miguu halafu akamkabidhi mzigo wake na kupokea fedha
“Jamani ni wakubwaaa” alisema Tricia baada ya kuwaona samaki
“Ndio...tena hapo bado, nitakuletea wengine wakubwa sana...mwanangu Maulid alikusifia sana anasema unampenda”
“Hahaa...jamanii”
“Ndioo...nashukuru sana Tricia ngoja mi niondoke”
“Ah mmh...dereva wako yuko wapi?”
“Yule kule anacheza na pikipiki”
Tricia alichungulia akamuona kwa mbaali, jamaa anatimua vumbi tu wala hajui kama Tricia yuko Mbeya, stress kwishney analelewa mjini anasubiri tu kuota kitambi.
Tricia akawa anampungia lakini wapi jamaa hamuoni ndipo akamuuliza Samawati
“Ni mume wako? Maana jana niliwaona pale hotelini mkiwa mna....hahaha” aliona aibu
“Hahahaa...hapana ni bwana wangu tu, naishi naye...tunasaidiana..ila ninampenda ni mstaarabu anajua sana kuishi na mwanamke, hana mbwembwe na wanawake wengine...kwa kifupi nilimpenda mwenyewe na najikuta nazidi kumpenda kila kukicha ndo nakolea maana napata mapenzi ya dhati ambayo niliyakosa kwa muda mrefu”
Samawati alijielezea kinaga ubaga bila kujua kwamba kadri anavyomsifia Maulid, ndivyo anavyouumiza moyo wa Tricia
“Haya...basi niwatakie safari njema”
“Poa”
Tricia aliingia ndani akiwa anazidi kuteseka moyoni licha ya kuwa ana mwanaume mwingine tena....JE NINI KITAFUATA USIKOSE KIPENGELE CHA 08
KIPENGELE CHA 08
Baadaye Samawati na Maulid walikuwa katika usafiri wanaelekea zao Nyasa kama ilivyokuwa ada....binti akasema
“Hivi kumbe wewe ni dereva mzuri kabisa”
“Sana...nilikuwa naendesha gari la mkaa toka njombe mpaka Dar”
“Mmmh...sasa kwanini ile gari yangu uwe unanichukulia mzigo mpaka sokoni?”
“Leseni imeisha muda wake...na kurenew ni elfu sabini na viposho posho lazima niweke laki chini”
“Sawa. Sasa sikia mi nitakupa hiyo pesa uka-renew leseni halafu unaanza kuwa dereva wangu ili kurahisisha kazi”
“Itabidi nichukue room...natamani niwe na maisha”
“Hivyo utafanya baadaye, mi si nitakuwa nakulipa kila tripu?”
“Basi hamna shida”
Samawati alimtazama Maulid halafu akamlalia begani, anajibebisha ili angalau azidi kupewa nafasi akamuambia “Nahisi kitu kimeshaingia huku nasikia kama kuna kautofauti mwilini”
“Itakuwa vizuri...”
Wakati wao wakibebishana, Tricia alikuwa ameketi kitandani, kashika tama, yale maneno ya Samawati yanajirudia rudia kwenye ubongo wake
“Hahahaa...hapana ni bwana wangu tu, naishi naye...tunasaidiana..ila ninampenda ni mstaarabu anajua sana kuishi na mwanamke, hana mbwembwe na wanawake wengine...kwa kifupi nilimpenda mwenyewe na najikuta nazidi kumpenda kila kukicha ndo nakolea maana napata mapenzi ya dhati ambayo niliyakosa kwa muda mrefu”
Akawa anatokwa na machozi taratiibu hajui hata yanatokea wapi. Alichukua mto akaupiga kitandani paah halafu akasema “Kumbe hukunipenda umenisahau kabisa, hata uko bize kumpa mapenzi mwanamke mwingine??” alisema binti yeye alikuwa haoni kwamba amemsahau hadi akatoka na Frank, alijiona yeye yuko sahihi kabisa.
Alifuta machozi na kusema “Hata hivyo sikutaki...sikutaki sikutaki mimi” roho ilikuwa inauma, alitamani hata asingemuona katika maisha yake yote “Nitakuonyesha” binti aliongea huku akiwaza afanyaje ili aweze kumuumiza Maulid.
*
SAA 12 JIONI
Frank alirudi nyumbani kama kawaida yake, halafu alimkuta binti kalala kadhoofika kitandani akamchangamkia
“Hi...baby”
“Vipi?” Tricia alisema huku akiijinyoosha kitandani na kujitathmini
“Safi” Frank aliongea huku akitazama jikoni yaani alivyopaacha asubuhi ndivyo hivyo kulivyo...kilichoongezeka ni samaki wawili wabichi wapo kwenye sufuria
“Kha vipi leo hujapika?” aliuliza
“Daah...sijisikii poa” alisema binti
“Haujisikii poa, unaumwa?” aliuliza Frank
“Hata sielewi...yani najisikia tu hovyo, nimelala sana tangu asubuhi...nilichoka sana usiku”
“Okay sawa....leo lakini hauendi”
“Yeah....si ndo mpaka kesho ndo naanza mchana”
“Okay”
Frank aliingia bafuni akaoga kisha akarudi na kujirusha kitandani....alipojaribu kumgusa binti alikataa, alikuwa hajisikii kuwa karibu na mwanaume kimapenzi.....mapenzi ni saikolojia, mtu huweza kumkataa hata mwenza katika ndoa kwa sababu ana stress za mchepuko.
“Hauko sawa. Au asubuhi nilikuboa?” aliuliza Frank maana alikumbuka kwamba asubuhi yake walikuwa wamegombana pale hotelini mara tu baada ya binti kumuona Maulid akilishwa kipande cha nyama
“Hamna...wala tena nahisi mi ndio nilikukosea”
“Hamna basi usijali...naomba unikumbatie tupumzike halafu tujue tunapika hizi samaki au la”
Tricia alimsogelea taratibu wakakumbatiana, lakini huwezi kuamini akili ya Tricia ilikuwa kwingine kabisa.
BAADA YA WIKI
Ikiwa siku ya ijumaa jioni Tricia alikutana na Samawati sokoni, Samawati akampatia samaki kama zawadi halafu wakawa wanapiga story mbili tatu
“Leo mjini uko peke yako?” aliuliza
“Hamna...nipo na shemeji yako amechoka...kuna sehemu kapumzika”
“Wapi...?” binti aliuliza
“Hahaha...unaulizia, hivi mnajuana au?”
“Hapana hatujuani. Ila naipenda couple yenu”
“Ah mh...yuko kule hotelini kwa siku ile amepumzika”
“Sawa... mtoto wako vipi nyumbani anaendelea vizuri lakini?” aliuliza Tricia maana yake mtoto Maulid alikuwa amesharuhusiwa kutoka hospitalini
“Ndio...anacheza sana na wenzake....hata shule anaenda sasa...namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kumjaalia afya”
“Haya sawa...ukienda kumuona muambie Dada Tricia anamsalimia”
“Hamna shida”
“Oh sawa....basi nikushukuru tutaonana Mungu akipenda”
“Hamna shida mdogo wangu
Plan kubwa ya Tricia alitaka kumuumiza Maulid, alikuwa hataki kuteseka peke yake, alienda nyumbani kulala ila alijua asubuhi ikifika lazima atampeleka hotelini mtaalam Frank kwa sababu ingekuwa ni siku ya mapumziko kwa wote wawili.
Alipika wakala na kulala....ilipofika asubuhi saa kumi na mbili, Tricia akaanza kumsumbua Frank
“Amka twende tukanywe supu kule hotelini” alisema
“Aaaah Baby...hadi siku ya mapumziko kuamshana mapema kweli?” aliuliza
“twende bhana” alisema binti huku akimvuta “Amka tukaoge, ninataka nikakufanyie surprise”
“Aaaah bana si tuende hata saa tatu?”
“Frank amkaaaa” binti alimsumbua mpaka jamaa akaamua kuamka
Walioga halafu wakaswaki na kuvaa vizuri haoo wakatoka kuelekea hotelini.
Kama ilivyokuwa imepangwa, Tricia alihakikisha ameketi kwenye meza moja na Frank halafu wakaagiza vya asubuhi...hata hivyo haikuchukua muda sana, Maulid pamoja na Samawati walishuka kutoka ghorofani wakaja kupata kifungua kinywa chini hotelini....ndipo Maulid akaketi bila kupepesa macho.
Tricia moyo ulikuwa unamuenda mbio, akachukua kipande cha nyama makusudi anamfanyia Frank kama Maulid alivyofanyiwa siku, ile lakini Maulid hakuona ila Samawati ndio aliona.
Macho ya Tricia na Samawati yalipogongana, ilibidi Samawati amchangamkie “Tricia...mambo”
Ndipo Maulid akageuza shingo na kumkuta Tricia pale akiwa na mwanaume mwingine tena wanaonekana kabisa ni wapenzi
“Safi dada kwema?” alisema binti na kutazama macho ya Maulid yaliyokuwa yakimtazama bila hata kuonyesha kushtushwa na kumuona pale.
Tricia kidogo alishangazwa na ile hali.... Maulid hakutaka hata kumchangamkia wala hakuonyesha kama ni mtu ambaye alishawahi kuwa naye katika mahusiano kipindi cha nyuma
Alirudisha macho pembeni na kumuuliza Samawati “Umeshaagiza?”
Tricia akabaki anashangaa kwanini jamaa hajali???.....ITAENDELEA
KIPENGELE CHA 09
Utamu wote wa kunywa supu ulimuisha binti, alijua anamkomoa mwanaume kumbe mwanaume mwenye hata hamkumbuki, na hata kichwani mwake hajamuweka kabisa. Tricia alijisikia maumivu makubwa na alihisi amedhalilika.
Aliacha zoezi lake la kunywa supu akabaki anamtazama, Maulid hana hata muda naye ndo kwanza anakunywa supu taratibu huku akipiga story na Samawati.
Baadaye Samawati na Maulid walipanda juu ghorofani, walitaka wapumzike wikiendi nzima pale mjini.
Walipofika chumbani Maulid akamuuliza
“Uliyeniambia ameipenda couple yetu, ni yule msichana pale?”
“Ndiyo,,...ndiye nesi aliyekuwa anamjali sana mwanangu Maulid kipindi akiwa hospitalini”
“Anhaa”
“Vipi mnafahamiana au umejuaje kwamba ni yeye?”
“Hamna,...niliona jinsi mlivyochangamkiana nikajua lazima atakuwa ni yeye” aliongea Maulid huku akiinuka na kuvua shati, halafu akaingia bafuni
“Unaenda kufanyaje tena?”
“Si kuoga?”
“Kuoga, si umeoga asubuhi hii tu?” aliuliza Sama
“Ah...nilivyokunywa supu nili-sweat” alisema Maulid
“Mh haya”
Maulid aliingia bafuni akafungulia bomba la mvua halafu maji yakammwagikia taratiibu huku akianza kukumbuka mambo mengi sana.
Kumbe Maulid alivyomuona pale hotelini binti sio kwamba hakushtuka lakini alijizuia kwa kiasi kikubwa, akiwa bafuni hisia zilimpanda, alisikia hasira akapiga ngumi ukutani na kusema “Shit” halafu akavuta pumzi ndefu na kuinama...bado maji yakimtiririkia “Ina maana yule demu yuko Mbeya?? Ndio kila siku anawasiliana na Samawati?? Ina maana Tricia siku hizi kaajiriwi Mbeya?? Kwanini ananifanyia hivi?” alijiuliza na kuinua uso juu maji yakawa yanamtiririkia usoni akawa anawaza taratibu “Ina maana ana mwanaume siku hizi?” alijiuliza kwa hasira halafu akaanza kutokwa na machozi lakini yalikuwa yanaenda na maji kama ilivyo kwa samaki akiwa baharini.
Alioga muda mrefu sana... Maulid hakupenda kuonyesha maumivu yake mbele zawatu.....alijionyesha akiwa peke yake, hakika ilikuwa ikimuumiza sana kisaikolojia. Alijisikia upweke na asiye na bahati
“Kwa hiyo baba yake alininyima yule mwanamke mzuri kiasi kile?” alisema mtaalam kwa sauti ndogo kila alipokumbuka jinsi alivyokuwa anaangaliana naye pale hotelini muda wa nusu saa iliyokuwa imekatika.
“Pumbavu...bora nisingekutana naye” alisema mtaalam
Baada ya kujimwagia maji kwa muda mrefu sana, alitoka na kumkuta Samawati akiwa anaubembeleza usingizi maana usiku alikua na mikiki mikiki iliyomfanya asilale vizuri.
Maulid hakuweza kuvumilia akamuuliza “Huyu msichana ndiyo alikupatia simu siku ile kule hospitalini?”
“Ndio.....si ndo tulimpelekea samaki kule Itua??” aliuliza tena aisee hapo ndipo alipokosea kutaja mtaa aliokuwa akiishi mtoto wa kike.
Maulid alitulia kimya akashika tama, huku akimfanya Samawati kuendelea kusinzia moja kwa moja usingizini.
Baada ya Maulid kuhakikisha Sama amesinzia vizuri, aliinuka akavaa suruali na shati halafu akatoka speed kuelekea nje ya hoteli ndipo akachukua pikipiki
“Nipeleke Itua kiongozi”
“Poa”
Pikipiki ilitembea mpaka alipofika akashuka na kulitafuta geti la kina Tricia akagonga na alifunguliwa na mtoto mwenye miaka kati ya tisa au kumi.
“Hujambo?”
“Sijambo shikamoo”
“Marahaba...hivi Tricia anakaa hapa?” aliuliza
“Yule dada mmoja hivi....anafanya kazi hospitalini”
“Aaaah...mke wa ka Frank” alisema mtoto lakini hapo ndo kabisa alikuwa anazidi kutonesha kidonda cha mapenzi
“Huyo huyo...naomba umuambie kuna mtu anamuita” alisema
“Sawa”
Yule mtoto alienda kugonga mlango wa kina Tricia, ndipo akatoka Frank na kumuuliza “Vipi James”
“Eti dada yupo?”
“Yupo....” alisema Frank na kurudi ndani akamuita Tricia “Unatafutwa huko”
“Na nani tena”
“James”
Tricia alishuka kitandani na kusogea akafungua mlango na kutoka, dogo James licha ya udogo wake, alishusha sauti na kusema “Kuna mtu anakuita hapo nje”
Tricia akashangaa “Mimi?” dogo akatikisa kichwa.
Tricia alivaa ndala na kutembea hadi getini akachungulia, kuangalia hivi nje, mwamba huyu hapa ameegesha mkono mmoja getini halafu mwingine kashika kiuno.
Maulid aliinua macho akamtazama na kumuita “Tricia?” alisema huku akimuangalia, yaani kadri siku zinavyosogea ndio anazidi kuwa mzuri kupita maelezo
“Maulid” binti aliita huku akitoka na kufunga geti asije akasikika huko ndani
Maulid alimtazama binti kwa sekunde nyingi bila kuongea chochote....machozi yakimtoka na kutiririka mashavuni
“Mbona umekuja hapa?” binti aliuliza huku akitazama yale machozi yanavyomtoka
“Tricia...umeamua kuniumiza?” aliuliza mtaalam
“Kukuumiza kivipi?”
“Unafikiri sijashtuka? Unafikiri sijaumia nilivyokuona pale hotelini?......ina maana umeamua kuja kunioshea na huyo mume wako si ndio Tricia???.....daaaah?” alisema kwa uchungu Maulid na kufuta machozi
“Maulid....ondoka”
“Siondoki...” Maulid aliweka mgomo...machozi ni mengi, maumivu aliyokuwa anayasikia sio ya nchi hii....”Basi mwambie aje aniue kama alivyotaka kuniua baba yako ili mkae kwa amani maana mimi nimekuwa wa kuteseka tu”
“Maulid” binti alibaki tu akimuita jina halafu akamvuta kwa nguvu akampeleka sehemu ya mbali kidogo na pale getini ili asikutwe “Kwanini umekuja huku sasa? Nimekuona una mwanamke wako...tena mmelala wote hotelini muda mara nyingi...ni rafiki yangu yule”
“Hata kama....mi kwani nilijua upo Mbeya? Tricia nimeumia sana...mpaka nimelia”
“Kulia sio tatizo.....naomba usirudi tena hapa...endelea na maisha yako na mwanamke wako...na mimi naendelea na maisha yangu na mwanaume wangu”
Maulid alimtazama kwa hasira....hakuamini yale maneno yanatoka kinywani mwa Tricia, aliumia sana.
Sawa hakuwa na kitu, cha kuweza kumtunza lakini alimpenda sana mtoto yule mwenye asili ya kinyakyusa
JE MAULID ATACHUKUA HATUA GANI?? USIKOSE KIPENGELE CHA KUMI
FURAHA YANGU ILIPO
SEASON TWO 10 HADI 12
Na Mr AB ENTMENT
KIPENGELE CHA 10
TULIPOISHIA
“Hata kama....mi kwani nilijua upo Mbeya? Tricia nimeumia sana...mpaka nimelia”
“Kulia sio tatizo.....naomba usirudi tena hapa...endelea na maisha yako na mwanamke wako...na mimi naendelea na maisha yangu na mwanaume wangu”
Maulid alimtazama kwa hasira....hakuamini yale maneno yanatoka kinywani mwa Tricia, aliumia sana.
Sawa hakuwa na kitu, cha kuweza kumtunza lakini alimpenda sana mtoto yule mwenye asili ya kinyakyusa
ENDELEA
Tricia alimtazama Maulid kwa muda wa sekunde kadhaa, Maulid alikua amepungua kiafya, hata uso ulionekana kutokuwa na furaha kama ilivyokuwa mwanzo, hakujua tatizo limetokea wapi.
“Msssssiiiew” Maulid alisonya kwa hasira halafu akageuka na kuondoka zake kuelekea mjini tena kwa miguu.
Tricia naye alirudi ndani akamkuta Frank ameketi kitandani kanuna tayari
“Ulienda wapi?” aliuliza
“Ah...mh...ah kuna mtu nilikuwa naongea naye hapo getini”
“Mtu gani?”
“Ni ndugu yangu mtoto wa baba mdogo Isaac”
“Au sio...kwa hiyo ndio mkaondoka si ungemkaribisha ndani sasa?”
“Ahh...mh alikataa kuingia ndani”
“Unavyoongea tu unaonekana muongo...” alisema Frank
“Haki ya Mungu ni ndugu yangu, ina maana hauniamini?”
“Ok sawa”
Frank alitulia kimya, lakini kiukweli kitendo cha Maulid na Tricia kuonana kwa mara nyingine ingeweza kuleta madhara makubwa katika mahusiano ya Frank pamoja na Tricia
*
Mjini bata liliendelea kati ya Maulid na mama Maulid....round hii walihamia Soweto kabisa kwa Samawati alipokuwa amepanga nyumba nzima, kulikuwa hamna uoga, tayari tumboni kulionekana kuna kitu kimeanza kumsumbua Samawati kwa sababu mwezi na wiki mbili zilikuwa zimeshakatika.
Mara nyingi Tricia na Maulid walikumbana mjini wakiwa kila mmoja amefuatana na mpenzi wake mpya, lakini siku moja Frank alipata wasiwasi akamtokea Maulid njiani na kumsimamisha
“Samahani broo”
“Bila samahani”
“Naomba nikuulize”
“uliza”
“hivi kati ya unafahamiana na Tricia kivipi”
“Aahahaa...nilipokuona tu nilijua hilo ndo swali lako...” aliongea kwa matambo mtaalam na kumshika Frank begani “Nikuambie kitu kimoja tu mdogo wangu....mimi ni ex wa Tricia, na mimi ndiye nimemkata utepe yule mtoto...usijione una demu...kama alishawahi kukuambia kuhusiana na Maulid basi mimi ndiye” alimaliza sentensi akamuachia halafu akaendelea kutembea huku akicheka kwa dharau.
Frank alibaki ameganda kama sanamu anamuangalia tu Maulid alivyokuwa anatamba, ndipo akajisemea moyoni “kwa hiyo kumbe ndiyo huyu, ndo maana Tricia haeleweki kabisa”
Ilibidi tu aende nyumbani akapumzike huku akimsubiri Tricia maana alikuwa akienda mchana na Frank usiku. Tricia alipofika tu nyumbani hivi alipokelewa na maneno
“Kumbe ndo maana hueleweki siku hizi Tricia”
“Hee nini tena?”
“Nimekutana na Maulid, ananioshea mbaya...anatamba ndio alikutoa bikira...kumbe ndo maana unanifanyia vituko”
“Mmekutana wapi? Mi sawa kanitoa bikira, sasa anafikiri ndio kigezo cha kunitoa kwako? Anafikiri akishakuambia alifanya hivyo ndo nitarudiana naye mimi?”
“Acha mambo yako...mbona tangu ulipomuona tu umebadilika....hata tukikutana naye huwa unakosa confidence”
“Frank” binti aliita kwa hasira
“Nini?”
“Niache...sitaki maneno na wewe...wala sihitaji kurudiana na huyo bwege mimi”
“Ah” Frank alionekana kutokuamini maneno ya Tricia kabisa. Alihisi siku sio nyingi lazima atasalitiwa tu.
*
Kwa upande mwingine, mtalaka wa Samawati, ambaye anaitwa Iddi Mponela alikuwa amekaa na rafiki yake aitwaye Jumbe Bashiru walikuwa wakipiga story
“Ila mama Maulid kaiva siku hizi kulaleki?” alisema Jumbe
“Kaiva kivipi”
“Yaani kanoga kinoma, wowowo kama yote kuna jamaa ndo anazunguka naye kila mahali ndiyo nasikia anakula na analala kule Soweto” alisema Jumbe
“Acha matani...ni kweli alikuja hapa alikuwa amenoga lakini mi mwenyewe huwa najipigia tu...mwanamke ukishazaa naye ni ngumu kukunyima utamu mdogo wangu” alisema kwa wivu Iddi Mponela licha ya kuwa ameshampa talaka miaka zaidi ya mitatu imeshapita
“Ni kweli aise...mi mwenyewe mama Jafari nilimuacha kwa sababu hiyo hiyo....akikutana na baba mtoto wake anampa tu nyoko zake”
“Hahahaa....” Iddi alicheka sana
Kidogo Iddi alikuwa ni mtu mwenye ukatili mwingi sana alisifika katika unyanyasaji, hata sababu ya mtoto wake mkubwa (Maulid) kulazwa hospitali kwa wiki tano mfululizo, ilikuwa ni Iddi alimtandika vyema kwa sababu dogo alimwaga sukari kilo.
Hata hivyo baada ya kupewa taarifa kwamba kuna jamaa anakula ua lake la zamani hakuweza kuvumilia, baada ya Jumbe kuondoka, Iddi alimpigia simu mtalaka wake
“Mama Maulid” alisema Iddi baada tu ya Samawati kupokea simu
“Niambie unaendeleaje”
“Safi tu...nasikia umeamua kumuoa kijana unalea tu siku hizi”
“Kha...nani kakuambia?”
“Ulidhani sitajua? Tabia yako ndio ile ile hutaki kubadilika?” alisema Iddi kwa hasira
“Khaaa....una wazimu wewe Iddi ee? Unanionaje? Mimi na wewe si tushaachana unadhani mi sisikiagi hamu? Si upo na mke wako umeoa mimi unanifuatilia wa nini? Niache na maisha yangu”
“Nakuambia hivi...acha umalaya”
“We ms*** nini...umalaya uache wewe sio mimi...upo?” aliuliza
“Unanitukana?”
“Achana na mimi” alisema binti na kukata simu kwa hasira
Iddi alifura hasira, alivuta sigara kwa fujo, halafu jioni ilipofika akaamua kukusanya vijana wake watatu waendesha bodaboda halafu akaenda nao mpaka kule Soweto kumuonyesha binti yeye nani.
Kwa bahati mbaya sasa, walimkuta Maulid, Jawabu na binti wa kazi wakiwa barazani wanaongea ongea Iddi akauliza
“Mama Jawabu yuko wapi”
Binti wa kazi akajibu “Ameenda dukani anarudi”
“Pumbavu...” alisema na kumnyooshea rungu Maulid ambaye alikuwa amemshika Jawabu “Wewe unafanya nini hapa?” aliuliza Iddi huku akimtazama kwa hasira ndipo Maulid akashtuka akagundua kuna shari inaanza
“Nik.....ni...ni...” alipata kigugumizi cha ghafla hajui anatakiwa ajibu nini...
“Jawabu ondoka hapo” alisema Iddi kwa hasira ndipo jawabu akamkimbilia binti wa kazi
“we ndiye bingwa wa kutembea na wake za watu sio?”
“Bro...mimi si...si”
“Acha ufala...huyu demu unafikiri kajizalisha mwenyewe?” aliongea Iddi akimsogelea Maulid amekaa akamtandika kwanza kibao Maulid akaona nyota nyota na kudondoka kutoka kwenye kiti hadi kwenye sakafu....ITAENDELEA
KIPENGELE CHA 11
Binti wa kazi alibaki ameshika mdomo anashangaa kipi kimetokea
“Broo nini bwa...” kabla hajamalizia sentensi, Iddi alimtandika rungu moja mgongoni Maulid akapiga kelele kama mwehu “Mamaaaaaaa...auwiii” alisema huku akijiviringa chini akihangaika kwa maumivu
Wale vijana wengine wakamvamia na kuendelea kumshindilia mateke, ngumu, fimbo na marungi bila kujali wanapiga sehemu gani ya mwili, hakika maumivu yalikuwa ni makubwa mno, huku matusi ya kila aina yakitoka kinywani mwa watu hao.
Ilibidi binti wa kazi apige yowe, na ndipo watu wakakusanyika, na kumtoa Maulid akiwa hoi ameshapoteza fahamu damu zinamtoka kila mahali.
Bodaboda na pikipiki ziliondoka eneo la tukio....ndipo binti Samawati alikuwa anafika anashangaa watu wamejaa nyumbani kwake.
“Kuna nini jamani?” aliuliza
“Mama....baba Jawabu kaja kampiga anko Mau” alisema binti
“Auwiii.....auwiiii....huyu mwanaume ananitaka nini jamani” alisema Samawati akiweka mikono kichwani kwa kuchanganyikiwa, Maulid alikuwa amelala chali kama mtu aliyekufa
Sama alimuwahi na kumshika akamuita “Maulid....Mau.....” lakini mtu hakuitika
“Awahishwe hospitalini” alisema mwanaume mmoja
“Jamani tupate usafiri”
Harakati zilianza kumpeleka hospitali, dakika chache tu wakapata gari ya kujitolea akapelekwa hospitalini alipofikishwa tu hivi katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mbeya, aliingizwa wadini na kuanza kupatiwa matibabu.
Aliyekuwako pale, ni Frank siku hiyo mchana maana Tricia alitakiwa aingia shift ya usiku. Frank alikuwa anamjua, lakini madaktari wasingethubutu kumuachia mwanafunzi asaidie kutoa tiba, hivyo yeye aliangalia tu jinsi kazi inavyoendeshwa pale.
Samawati alilia sana, alichanganyikiwa, akatundikiwa dripu mtaalam, huku akiwa amepoteza kabisa usingizini kama aliyekufa.
Baadaye jioni...Frank alirudi nyumbani, akamkuta Tricia ameshajiandaa naye aende night, Frank hakutaka kumuambia chochote maana pia kulikuwa na ugomvi kati yao kwa sababu ya Maulid.
Waliagana na binti alienda hospitalini, alipofika tu hivi alikuta majukumu yake ya kila siku, ndipo nesi mmoja akamuomba amsaidie kwenda kubadilisha dripu katika chumba alichokuwa amelazwa Maulid.
Binti alichukua ile dripu kwa kiburi, maana aliona anapewa majukumu yasiyo ya kwake, akaenda bila hata kutazama ni jina nani, lakini alipofika alimkuta Maulid akiwa amelala chali ametundikiwa dripu na yupo na housegirl ambaye Tricia alikuwa hamfahamu kabla, huku Samawati akiwa kituo cha polisi anatoa taarifa la tukio alilolifanya Iddi na wenzake.
Tricia alibadilisha dawa kwenye dripu halafu akaanza kupiga hatua kuondoka aende nje ila kichwani likamjia wazo “Hapa ninajifunza, yaani naondoka hata sijui huyu mgonjwa kapatwa na nini....” alisema na kugeuka akamtazama yule msichana wa kazi akamuuliza “Hujambo?”
“Sijambo” alisema binti na kisha kupeleka jicho kwa mgonjwa alipotazama usoni hivi alishtuka kidogo na kutoa macho halafu akasogea na kutazama vizuri.
Alipotazama akagundua sio mtu mgeni kwakem na tena ndevu ni kama zile zile za Maulid. Akasogea vizuri na kumtazama usoni amepigika kisawasawa “Maulid” aliita kwa mshangao binti kisha akamgeukia binti wa kazi “Wewe.....huyu si Maulid huyu?” binti wa kazi akatikisa kichwa kumaanisha ndiyo ni yeye.
Tricia alishtuka maana mwanaume huyo alikuwa anatembea na roho yake, alijikuta anaweka tray chini likalia parakatan....halafu akaketi kitandani na kumtazama vizuri “Amepatwa na nini?” aliuliza Tricia, huwezi amini licha ya kujua kwamba yule mwanaume ana mwanamke mwingine, bado aliishi rohoni mwake, alikuwa amemkaa kisawasawa na kumtoa ilikuwa ni ngumu.....bila hata kutarajia machozi yalianza kumtoka “Ame...patwa na nini??” aliuliza huku akimtazama binti wa kazi yeye anashangaa tu nesi analia nini maana hakujua kuna siri kubwa
“Eti....mmefanya nini Maulid jamani?” alizidi kulalamika na kumshika kichwani Maulid hayupo....roho yake imekaa pembeni kabisa inasubiri muda wa kurudi au ikiamua iondoke mazima akazikwe
“Amepigwa” alisema binti wa kazi
“Na nani???....nani amempiga Maulid?” Tricia alianza kumfokea binti kwa hasira utafikiri yeye ndo amempiga akamtikisa “We Maulid....wewe..umelala??” aliuliza
“Amepoteza fahamu” alisema binti wa kazi
“Aaaah” Tricia alijikuta anapagawa na kuinuka akatoka haraka anaenda kule kwenye chumba cha daktari “Doctor”
“Nini tena?”
“Yule mgonjwa wa chumba kile anaumwa sana jamani...anahitaji msaada wa harakaa....anatakiwa apone” alisema binti huku machozi yakimtoka bado....doctor akashangaa
DAAAA YAAANI HAYA MAPENZI NI MABAYA SANA
KIPENGELE CHA 12
Doctor alimtazama Tricia kwa sekunde kama kumi anajifuta machozi, daktari haelewi ni mgonjwa gani anamliza, ikabidi aanze kutafuna kifuniko cha kalamu halafu akamuuliza “Mgonjwa gani huyo?”
“Yule wa wadi ya wanaume....kitanda namba saba” alisema
“Mh kwani ni nani yako mbonau unalia?”
Binti alishika vidole kwa aibu halafu akasikitisha kichwa na kusema “Hamna....” alisema kwa aibu
“Ngoja tunasubiri aamke ndiyo tunaweza kumuhudumia vizuri”
“Sawa”
Tricia aliondoka kinyonge, usiku ulikuwa m-baya kwake na hata kujikuta anashindwa kufanya kazi vizuri kama siku zingine, kila muda anafikiria imekuwaje.
Muda huo huo Frank akampigia simu, binti akapokea “Vipi??”
“Safi, hapo hospitalini kunaendeleaje?”
“Subiri nitakutafuta bwana” alisema Tricia na kukata simu Frank akabaki anacheka kwa sababu alijua kwamba binti ameshakutana na moto huko.
Frank yeye kwa upande wake alikuwa anafurahi maana aliona mpinzani wake akiteseka ndio akafurahi, ni sawa na shabiki wa Simba SC anavyojisikia furaha pale wa Yanga SC anavyoteseka, au wa Yanga SC anafurahi sana pale wa Simba SC anapokuwa akiteseka, furaha ya upinzani kumuona mpinzani hafurahii maisha.
*
Upande mwingine ni marungu yalikuwa yanatembea kwa Iddi na kijana wake mmoja ambaye walishirikiana kumvamia Maulid, maana walikuwa kwenye mikono ya Jeshi la Polisi usiku ule, lakini wawili bado walikuwa hawajapatikana kwani walikuwa wameshatoroka mjini Soweto, ndani ya Jiji la Mbeya.
Baada ya kuwasweka sero, ndipo Samawati alipata nafasi ya kuja na chakula hospitalini na alipofika alikuta binti wa kazi alikuwa nje kwenye kiti cha mapokezi, ikabidi aingie ndani akamkuta Tricia akiwa na mgonjwa kando mwa kitanda anamtazama huku akisali kimoyo moyo asije akafa.
Alipomuona Samawati, binti aliinuka na kusema “Dada”
“Mdogo wangu uko hapa?”
“Ndio....vipi imekuwaje tena mbona wamempiga hivi?”
“Jamani huyu ni mtalaka wangu, baba Maulid ndiye ameamua kumpiga hivi, kisawa wivu” alisema Samawati
“Kweli?”
“Ndio”
“Jamani nusu amuue” alisema binti, unajua alikuwa anampenda Maulid sio mchezo...yani alikuwa anampenda sana sana sana sana.
Usiku ulipozidi, Samawati ilibidi aondoke, akamuacha mgonjwa mikononi mwa madaktari, maana yeye alikuwa na Jawabu pamoja na binti wa kwazi, wote ni wadogo, hakujua afanye nini.
Usiku kwenye saa nane, Tricia ameketi kando ya mgonja ameshika mkono wake anauchezea huku akisema “Eeh Yesu wangu naomba umuamshe Maulid....naomba umuamshe eh Bwana” alisema mtoto wa kike..
Muda huo daktari yuko mlangoni anamchungulia binti vitu anavyofanya, akasikitika na kusema “Huyu atakuwa anampenda...lakini mbona kama vile yeye na Frank ni wapenzi? Ina maana anapenda wote” aliongea huku akitembea kuelekea nje ya jumba la hospitali.
Tricia baada ya kusali zake alienda chooni kujisaidia, sasa wakati anarudi alimkuta Maulid kakodoa macho kweli kweli anashangaa, binti akashtuka na kumuwahi
“Maulid umeamka?”
“Niko wapi?” aliuliza Maulid huku akimshangaa binti usoni kama sekunde thelathini ndio akamtambua “Tricia” alimuita
“Abee....ngoja nikuite daktari” alisema huku akitoka na kukimbia akimuita daktari “Doctor....doctor” mpka akampata
Huku nyuma alimuacha Maulid akiwa anajaribu kunyanyua mkono anashangaa maumivu ni makali, ndio akaanza kuvuta kumbukumbu na kukumbuka mara ya mwisho alikuwa wapi
“Khaaa...ina maana niko hospitalini?” alijiuliza na kujaribu kuinuka, anaumwa kila mahali.
Daktari alifika pale akamuhoji hoji maswali na kumfanyia vipimo halafu akamuambia Tricia aondoke pale ndani asiendelee kukaa
“Kwanini doctor?” aliuliza Tricia
“We nenda tu” alisema
“Naomba umuache please doctor” alisema Maulid
Daktari aligundua kuna jambo linaendelea kati ya watu wale wawili ndipo akachukua daftari lake na kuondoka akawaacha.
Tricia aliketi kando ya Maulid halafu akamtazama, ila Maulid akawa anatazama juu darini, ndipo machozi yakaanza kumtiririka huku akilaumu
“Kwani mimi nimemkosea nini Mungu?? Nimeikosea nini dunia?”
Tricia naye akaunga, anaanza kulia “Usilie Maulid...mbona hivyo?”
“Hapana Tricia ninateseka sana, kila nikikaribia kupata furaha yananitokea mambo ambayo yananitoa kwenye furaha moja kwa moja...naumia sana sana sana”
“Maulid” alisema binti huku akimshika kichwani kwa kumbembeleza “Naoma uwe mpole, maumivu yameumbwa kwa ajili yetu sote, sitamani kuona machozi yako, wewe ni mwanaume”
“Sawa mimi ni mwanaume.....lakini nimeshazidiwa...kila nikijaribu njia yoyote ya mafanikio najikuta naangukia pua, narudi kwenye sifuri” alisema Maulid
“Pole.....pole Maulid unanifanya mimi nilie eti??”
“Usilie Tricia, daa nyingine bora mtu ufe tu kuliko haya mateso nayopitia...nimeteseka, sina mzazi na sina ndugu wa kutegemea, baada ya kupoteza ada ya kwenda chuo cha sheria walinitelekeza ndugu wote”
“Pole Maulid....” binti alijaribu kumtia moyo “Ipo siku tu utafanikiwa usiumie”
“Nalia kwa sababu ya mengi”
“Usiwaze sana Maulid, unajua mpaka umekonda? Sasa kwanini uliacha ile kazi yako ya mkaa?” aliuliza binti
“Tricia huwezi ukaelewa.....hutoelewa” machozi yalizidi kumtoka kijana wa watu
“Basiii” binit alibembeleza
“Ona...nikitoka hapa hospitalini sina pa kwenda kukaa, sina nyumba, sina hata godoro...naenda wapi mimi nikiwa mgonjwa hivi?” aliongea kwa huzuni sana kijana Maulid, alishaozea maisha ya kuishi bila sehemu maalum, lakini kipindi hiki alikua mgonjwa, nani angelimpokea?? Alijiuliza sana
Machungu yalipozidi, Tricia aliondoka polepole na kumuacha peke yake alie mwenyewe....naye alienda kulilia mbali
ITAENDELEAAA

Fundiii sanna mzee
ReplyDeleteNzuriii sanaaa
ReplyDeleteNouma
ReplyDelete